1 Wakaleta Sanduku la Mungu na kuliweka ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelisimamisha kwa ajili yake, na wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu.
2 Baada ya Daudi kumaliza kutoa hizo sadaka za kuteketezwa na hizo sadaka za amani, akawabariki watu katika jina la Bwana.
3 Kisha akamgawia kila Mwisraeli mwanaume na mwanamke mkate, andazi la tende na andazi la zabibu kavu.
4 Akawaweka pia baadhi ya Walawi ili wahudumu mbele ya Sanduku la Bwana kufanya maombi, kumshukuru na kumsifu Bwana, Mungu wa Israeli:
5 Asafu ndiye alikuwa mkuu wao, akisaidiwa na Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliabu, Benaya, Obed-Edomu na Yeieli. Hawa ndio wangepiga zeze na vinubi, Asafu angepiga matoazi,
6 nao Benaya na Yahazieli makuhani, ndio wangepiga tarumbeta mara kwa mara mbele ya Sanduku la Agano la Mungu.
7 Siku ile, kitu cha kwanza Daudi alichofanya ni kumkabidhi Asafu na wenzake zaburi hii ya shukrani kwa Bwana:
8 Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake;
9 Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa;
10 Lishangilieni jina lake takatifu;
11 Mtafuteni Bwana na nguvu zake;
12 Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya,
13 enyi wazao wa Israeli mtumishi wake,
14 Yeye ndiye Bwana Mungu wetu;
15 Hulikumbuka agano lake milele,
16 agano alilolifanya na Abrahamu,
17 Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri,
18 “Nitakupa wewe nchi ya Kanaani
19 Walipokuwa wachache kwa idadi,
20 walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine,
21 Hakuruhusu mtu yeyote awaonee;
22 “Msiwaguse niliowatia mafuta;
23 Mwimbieni Bwana dunia yote;
24 Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa,
25 Kwa kuwa Bwana ni mkuu,
26 Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu,
27 Fahari na enzi viko mbele yake;
28 Mpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa,
29 mpeni Bwana utukufu
30 Dunia yote na itetemeke mbele zake!
31 Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi;
32 Bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake;
33 Kisha miti ya msituni itaimba,
34 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema;
35 Mlilieni, “Ee Mungu Mwokozi wetu, tuokoe.
36 Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli,
37 Daudi akamwacha Asafu na wenzake mbele ya Sanduku la Agano la Bwana ili wahudumu humo mara kwa mara, kulingana na mahitaji ya kila siku.
38 Pia akamwacha Obed-Edomu pamoja na wenzake sitini na wanane wahudumu pamoja nao. Obed-Edomu mwana wa Yeduthuni na pia Hosa walikuwa mabawabu wa lango.
39 Daudi akamwacha kuhani Sadoki pamoja na makuhani wenzake mbele ya hema ya ibada ya Bwana katika mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni
40 ili kutoa sadaka za kuteketezwa kwa Bwana kwenye madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa mara kwa mara, asubuhi na jioni, sawasawa na kila kitu kilichoandikwa katika sheria ya Bwana ambayo alikuwa amempa Israeli.
41 Waliohudumu pamoja nao walikuwa Hemani, Yeduthuni na wale wote waliochaguliwa na kutajwa kwa jina kumpa Bwana shukrani, “Kwa maana fadhili zake zadumu milele.”
42 Hemani na Yeduthuni walikuwa na wajibu wa kupiga tarumbeta, matoazi na kutumia vyombo vingine kwa ajili ya nyimbo za sifa kwa Mungu. Wana wa Yeduthuni waliwekwa langoni.
43 Kisha watu wote wakaondoka, kila mmoja akarudi nyumbani kwake, naye Daudi akarudi nyumbani kuibariki jamaa yake.